John 6:15-20

15 aIsa akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke yake.

Isa Atembea Juu Ya Maji

(Mathayo 14:22-33; Marko 6:45-52)

16 bIlipofika jioni, wanafunzi wake waliteremka kwenda baharini. 17Wakaingia kwenye mashua, wakaanza kuvuka bahari kwenda Kapernaumu. Wakati huu kulikuwa tayari giza na Isa alikuwa hajajumuika nao. 18Bahari ikachafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma. 19 cWanafunzi walipokuwa wamekwenda mwendo wa karibu maili tatu au nne,
Maili tatu au nne ni kama kilomita 5 au 6.
walimwona Isa akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana.
20 eLakini Isa akawaambia, “Ni mimi. Msiogope.”
Copyright information for SwhKC